
1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS – TAMISEMI
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA WALIMU WA MASOMO YA
SAYANSI, HISABATI, LUGHA (LITERATURE IN ENGLISH) NA
FUNDI SANIFU MAABARA KWA AJILI YA SHULE ZA SEKONDARI
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
inawatangazia nafasi za kazi, Wahitimu wa fani ya Ualimu na Fundi Sanifu
Maabara za Sayansi kwa ajili ya Shule za Sekondari. Waombaji wa kazi
wanapaswa kuwa ni Wahitimu wa fani hizo wa mwaka 2017 au kabla ya
mwaka huo. Maombi yanapaswa kutumwa OR-TAMISEMI.
Sifa za waombaji wa nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:
1. Wahitimu wa Stashahada (Diploma) ya Ualimu mwenye kufundisha
masomo ya Sayansi. Mwombaji awe na somo la kufundishia la Fizikia
au Hisabati;
2. Wahitimu wa Shahada (Degree) ya Ualimu mwenye kufundisha
masomo ya Sayansi. Mwombaji awe na somo la kufundishia la Fizikia
au Hisabati;
3. Wahitimu wa Shahada (Degree) ya Ualimu kwa somo ya Lugha
Mwombaji awe na somo la kufundishia la Literature in English; na